VIGEZO NA MASHARTI YA
VODACOM CHEKECHA MKWANJA
1. UTANGULIZI
Vigezo na Masharti yafuatayo yanabeba mawazo ya dharura na/au majukumu unayochukua na ukomo wake na vinaondoa wajibu na majukumu ya kisheria ambayo Vodacom itachukua kwako na kwa watu wengine. Hivi Vigezo na Masharti pia vinaweka mipaka na kuondoa haki zako na suluhisho dhidi ya Wadhamini na vinakubebesha dharura, majukumu na wajibu wa kisheria. Hivi Vigezo na Masharti vinakusababisha wewe kuwajibika kulipa gharama na malipo ya ziada na Wadhamini wanaweza kutoa madai na madeni mengine dhidi yako.
Kwa kuwa Vigezo na Masharti au bidhaa au huduma zozote zinazotolewa chini ya Vigezo na Masharti hayo vinaongozwa na Kanuni, hakuna Vigezo na Masharti vilivyokusudiwa kupingana na masharti ya Kanuni zinazotumika.
Tafadhali soma kwa makini hivi vigezo na masharti na Vigezo na Masharti ya Jumla ya Mtumiaji wa Vodacom ambavyo vitakuwa sehemu ya hivi Vigezo na Masharti vilivyochukuliwa katika tovuti ya Vodacom.
Kushiriki kwako katika ofa hii kutamaanisha kuwa umekubali kufuata hivi Vigezo na Masharti. Iwapo hukubaliani na hivi Vigezo na Masharti, tafadhali usishiriki katika ofa hii, ni wajibu wako kupitia hivi Vigezo na Masharti mara kwa mara.
2. FASILI MBALIMBALI
Kampeni Tangazo litatolewa kwa wateja wa Vodacom ili waweze kujiunga na huduma hii na kucheza Chekecha Mkwanja.
Njia za Kushiriki Kampeni: Wateja wa Vodacom wanaweza kushiriki katika huduma ya Promosheni ya Chekecha Mkwnja kupitia njia zifuatazo SMS, Ukurasa wa www.chekechamkwanja.com
Mshiriki ni Mtumiaji wa huduma za promosheni za Vodacom Chekecha Mkwanja.
Zawadi: bonyeza hapa
Watoa huduma za masoko ni (i) Mdhamini; msambazaji wa bidhaa na au huduma kulingana na Promosheni hii; na wabia wa Promosheni, wachapaji, wakala wa matangazo na promosheni, washauri wa kitaalamu na wafanyakazi wa kituo cha mauzo walioajiriwa au walio na mkataba, au wanaosambaza bidhaa au huduma za aina yoyote, kwa watu wote au vyombo vilivyoorodheshwa hapo juu wakati wa Kipindi cha Promosheni.
Mshiriki ni mshiriki wa Kampeni mwenye sifa ambaye ni mteja wa Vodacom mwenye umri wa miaka 18 au zaidi.
Mdhamini ni Vodacom
Promosheni ni fursa ya kushiriki kwenye mchezo ambapo wateja watashinda tuzo kama ilivyoelezwa katika hivi Vigezo na Masharti. Mdhamini ana haki ya kuongeza muda wa mchezo na kurekebisha tuzo zinazotolewa.
Kanuni ni Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Ulinzi wa Mteja) 2018 (kamailivyorekebishwa mara kwa mara), na sheria nyingine zozote za Tanzania zinazotumika.
Huduma ni Vodacom Chekecha Mkwanja.
Vodacom Chekecha Mkwanja ni jina la kampeni na linajumuisha Huduma ya Chekecha Mkwanja.
Vodacom ni Vodacom Tanzania Public Limited Company.
3. AINA YA HUDUMA
Mchezo wa Chekecha Mkwanja wa Cheza na Shinda
Chekecha Mkwanja ni huduma ya uvumbuzi ambayo wateja watajibu maswali 9 kwa usahihi ili kushinda zawadi kubwa! CHEKECHA MKWANJA inaweza kuwa juu ya teknolojia, michezo, muziki, afya, au sayansi. Unapata kuchagua kipengele! Pia, unaweza kutumia njia tatu za kukusaidia wakati wa mchezo. Usifanye makosa na USHINDE jackpot.
4. Namna ya Kucheza na Kushinda
i. SMS: Tuma neno MKWANJA kwenda 15914
ii. Ukurasa:www.chekechamkwanja.com Gharama na Ushiriki kwa Mara ya Kwanza
i. Kushiriki mara ya kwanza (Kwanza tuma SMS/Ujumbe Mfupi kwenda 15914) utapokea ujumbe wa kuonesha umefanikiwa kujiunga, SMS kwa ushiriki kwa SIKU kwa kujirudia na ushiriki kwenye ukurasa gharami pia zitakuwa sawa na za SMS.
Zingatia: Kujirudia yenyewe “Auto renewal” hapa kila siku mtumiaji atatozwa moja kwa moja na huduma kujirudia yenyewe ili kuangalia na kushinda tuzo mbalimbali.
ii. Wateja wanakubali kuwa kwa kujiunga katika mchezo huu itawabidi kulipia gharama za kujiunga kwenye huduma za Chekecha Mkwanja kama ilivyotolewa kwenye tovuti yetu.
Washindi wataarifiwa kwa simu na Mdhamini na/au wakala wa Mdhamini wakati mwafaka au mapema iwezekanavyo baada ya kila droo.
Droo itaendeshwa moja kwa moja na droo kubwa itakuwa chini ya usimamizi wa Bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania.
Mteja anaweza kushinda tuzo za aina moja mara moja wakati wa promosheni kwa droo ya siku kwa wiki na mwezi watachukuliwa washiriki wenye pointi nyingi Zaidi.
Washiriki wanatambua na kukubali kuwa Mdhamini atatumia mtu wa tatu (wakala wa Mdhamini waliothibitishwa) kuwasiliana na mshiriki, iwapo mshiriki atakuwa mshindi; na kupanga namna ya kumpatia Tuzo. Ili kuanzisha mchakato wa kuwasiliana na kupeleka tuzo, Mdhamini atampatia mshiriki taarifa kupitia mtu wa tatu.
5. UWEPO NA UPATIKANAJI WA TAARIFA NA UTARATIBU WA KUJIONDOA
5.1 Taarifa zote kwa washiriki za Mchezo wa Promosheni zitachapishwa kwenye tovuti ya Vodacom Tanzania, Mitandao ya Kijamii ya Vodacom na kurasa za
- Instagram: vodacomtanzania,
- Facebook: vodacomtanzania,
- tovuti ya Vodacom: vodacom.co.tz
5.2 Kila mshiriki anaweza kujiondoa kwenye Mchezo wa Promosheni na kuacha kupokea taarifa yoyote kuhusu Mchezo wa Promosheni kwa kutuma SMS/Ujumbe Mfupi wenyeneno “STOP” kwenda namba 15914, www.chekechamkwanja.comau kupiga namba ya huduma kwa wateja 100 (bure) na kuomba atolewe kwenye kampeni. Iwapo baada ya hapo mshiriki ataamua tena
kutuma ujumbe mpya wa SMS kwenda Namba 15914 au MKWANJA kwa ajili ya trivia atafikiriwa tena kama mshiriki kwenye Mchezo.
5.3 Iwapo Mchezo wa Promosheni utasitishwa, Mdhamini wa Mchezo wa Promosheni atachapisha kwenye sehemu za machapisho rasmi ya Mchezo wa Promosheni na kutuma taarifa kwa SMS/Ujumbe Mfupi kwenda kwa wateja.
5.4 Katizo au usitishwaji mapema wa Mchezo wa Promosheni hautamwondolea Mdhamini jukumu lake la kutoa tuzo zilizotolewa kabla ya usitishwaji huo na kutekeleza hatua nyingine zinazotakiwa, isipokuwa kwa matukio ambayo ukatizaji au usitishwaji wa Mchezo wa Promosheni ulisababishwa na vitendo au matukio ambayo yapo nje ya uwezo wa Mdhamini.
5.5 Mdhamini wa Mchezo hatatoa taarifa kuhusu washiriki wa Mchezo wa Promosheni kwa mtu yeyote isipokuwa kama atatakiwa kufanya hivyo kisheria au ili kutekeleza maagizo ya vyombo vya serikali ya Tanzania.
5.6 Mdhamini ana haki ya kutoingia katika majadiliano kwa maandishi au kuwasiliana kwa njia nyingine yoyote na washiriki wa Mchezo wa Promosheni kinyume na Vigezo na Masharti au kulingana na matakwa ya sheria ya Tanzania.
5.7 Mdhamini ana haki ya kutoa bure namba za kutuma ujumbe wakati wote wa Mchezo wa Promosheni kwa madhumuni yoyote.
6. Mabadiliko ya Hivi Vigezo na Masharti
6.1 Tunaweza kuongeza au kubadili Vigezo na Masharti haya ya Matumizi kulingana na kifungu cha 6.2. Tunaweza kuongeza ada na tozo mpya au kubadili ada na tozo zilizopo wakati wowote; kutokana na sheria mpya, kanuni za kisheria, kanuni za Serikali au matakwa ya leseni, viwango vya kubadili fedha, kuanzishwa au kubadilishwa kwa kodi ya serikali au kutokana na mapitio yoyote ya mipango ya kibiashara ya Vodacom, mabadiliko ndani ya tasnia, mapendekezo kutoka vyombo vya usimamizi au kutokana na sababu nyingine itakayojitokeza.
6.2 Tutakutaarifu mapema ikiwa tunataka kuongeza au kubadili vigezo na masharti haya au ikiwa tunataka kuongeza ada na tozo mpya au kubadili zilizopo wakati au baada ya kujiunga na Huduma hizi. Kiasi cha malipo na aina ya taarifa tutakayokupa zitapitia njia mwafaka zinazotumika na kupatikana kwa wakati huo kwa mfano, tunaweza kukutaarifu kwa barua, barua pepe, simu (ikiwa ni pamoja na ujumbe uliorekodiwa au ujumbe wa simu ulioandikwa) au kwa matangazo katika gazeti la kila siku au kila wiki au katika tovuti yetu au njia nyingine yoyote). Unashauriwa pia kutembelea tovuti yetu mara kwa mara ili kuona mabadiliko hayo kama kwa sababu zisizotarajiwa inawezekana hukupata taarifa hizo.
6.3 Ikiwa hukubaliani na mabadiliko au nyongeza katika Vigezo na Masharti haya, unaweza kusitisha huduma hizi kwa mujibu wa kifungu cha 7 hapo chini. Ikiwa wewe hujatutaka tusitishe Masharti ya Matumizi na bado unatumia Huduma hizi, utachukuliwa kuwa umekubali mabadiliko hayo tangu yalipoanza kutekelezwa.
7. Kusitisha Huduma
7.1 Tunaweza kusitisha Masharti haya ya Matumizi wakati wowote tutakapoamua. Usitishwaji huo utafanyika baada ya kukupa Taarifa. Taarifa inaweza kuwa kwa barua, baruapepe, simu (ikiwa ni pamoja na ujumbe uliorekodiwa au ujumbe wa simu ulioandikwa) au kwa tangazo katika gazeti la kila siku au la kila wiki au kwenye tovuti yetu au njia nyingine yoyote. Unashauriwa pia kutembelea tovuti yetu mara kwa mara ili kuona mabadiliko yote yaliyofanyika, kama endapo kwa sababu zisizotarajiwa unaweza kuwa hujapata taarifa.
7.2 Unaweza kusitisha Masharti ya Matumizi/Huduma kwa kuacha kutumia Huduma hizi na Kujiondoa.
8. Mawasiliano na Malalamiko
8.1 Unaweza kuwasiliana nasi kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga nambari 100 au njia nyingine za mawasiliano ya huduma kwa wateja zinazopatikana katika mitandao yetu ya kijamii au Tovuti (yaani TOBi Online au Kutuma maswali) kutoa taarifa kuhusu migogoro, madai au tofauti zozote zinazojitokeza katika Huduma hizi.
8.2 Ikiwa hujaridhika kwa lolote kuhusiana na huduma zinazotolewa, tafadhali wasiliana na Kituo cha Huduma kwa Wateja. Watafurahi kukusaidia na kukufafanulia taratibu za kushughulikia malalamiko kwa undani. Tutajitahidi kushughulikia malalamiko yako mapema iwezekanavyo. Hata hivyo, mara nyingi malalamiko yatapaswa kufanyiwa uchunguzi. Kama hivyo ndivyo, tutakupa mrejesho ndani ya siku 7 za kazi kuthibitisha upokeaji wa malalamiko yako na muda wa tutakaotumia kuyashughulikia malalamiko hayo. Ikiwa malalamiko yako hayatapata ufumbuzi, utashauriwa namna ya kufanya.
9. Wajibu wa Kisheria
9.1 Hatutahusika kwa kuchelewesha au kushindwa kutekeleza majukumu yetu yoyote yanayohusu matumizi ya Huduma hizi ikiwa kuchelewesha au kushindwa huko kumetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu wa kutoa Huduma hiyo.
9.2 Huwezi kubadili Masharti haya ya Matumizi na huwezi kuhamisha vigezo hivi kwa mtu au biashara nyingine.
9.3 Masharti haya ya Matumizi yataongozwa na kufasiriwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
9.4 Hatutahusika kwa suala lolote linaloweza kusababisha hasara inayoendana na masharti haya.
9.5 Mawasiliano yote kuhusu Vigezo na Masharti haya yatafanyika kwa Kiingereza au Kiswahili.
10. MAELEZO YA JUMLA
10.1 Mdhamini, wakurugenzi wake, washirika, wajumbe, waajiriwa, wakala, washauri, wasambazaji, wakandarasi, kampuni tanzu na wadhamini hawawajibiki kwa hali yoyote kwa hasara ya moja kwa moja au kwa namna nyingine au uharibifu, ikiwa ni pamoja na ingawa haiishii katika madhara ya kimwili au kifo, kinachotokana na au kutokana na ushiriki wa mteja katika Promosheni au fidia ya Tuzo yoyote kuhusiana na Promosheni hii, au marekebisho yoyote ya maelezo ya Tuzo na/au vigezo na masharti ya Promosheni hii. Washiriki wote (pamoja na washindi) hapa wanaeleza kumlinda Mdhamini kwa hali hii hatawajibika na madai yoyote yanayotokana na sababu zilizoelezwa hapo juu.
10.2 Hivyo, kwa kuwa ni muhimu, inatakiwa na sheria au inazidi uwezo wa Mdhamini, Mdhamini ana haki ya kubadili aina ya Promosheni, Tuzo, au hivi vigezo na masharti baada ya kutoa taarifa na kuchapishwa kwenye tovuti ya www.Vodacom.co.tz au kwa njia nyingine. Iwapo Tuzo ni chache au tofauti kwa hali hii, Mdhamini atabadili Tuzo na tuzo inayolingana nayo kwa thamani.
10.3 Vigezo na masharti yoyote yatakayochapishwa kwenye chombo chochote cha habari au katika tovuti ya VODACOM website www.Vodacom.co.tz itatumika kuweka vigezo na masharti ya Promosheni, ambapo washiriki wanakubaliana kuyafuata.
10.4 Washindi watapatiwa taarifa kwa simu na/au baruapepe kwa kuzingatia taarifa za mawasiliano zilizotolewa na mshindi alipokuwa anaingia katika Shindano. Tafadhali zingatia kuwa washindi hawatapewa taarifa kwa SMS. Mdhamini atajaribu kuwasiliana na mshindi kwa muda wa siku 10 baada ya jina lake kuteuliwa kuwa mshindi. Iwapo ikitokea mshindi hapatikani (wakati uliotajwa hapo juu) au iwapo mshindi akikataa, au akigoma kupokea zawadi, zawadi hiyo itafanyiwa droo nyingine mpya. Zaidi ya hayo, iwapo Mdhamini akimpigia mshindi baada ya kushinda zawadi na mshindi hapatikani kwenye simu ili kuweza kumfikishia Tuzo Mdhamini ataendelea kujaribu kuwasiliana na mshindi kwa mara tatu (3) ndani ya siku na kama mshindi bado hapatikani, itachezeshwa droo mpya kwa droo ya siku ila kama ni wiki atapatiwa mshiriki wa pili mwenye point nyingi vivyo hivyo kwa zawadi kubwa.
10.5 Zawadi haiwezi kuhamishwa na haiwezi kubadilishwa na tuzo nyingine.
10.6 Uamuzi wa Mdhamini kuhusiana na migogoro inayotokana na Promosheni hii itashughulikiwa na Mdhamini kwa kuzingatia hivi vigezo na masharti. Uamuzi wa Mdhamini hapa utakuwa wa mwisho.
10.7 Washindi wanastahili kushinda Tuzo 1 (moja) kila moja katika mzunguko wa droo (yaani Tuzo moja kwa kila droo ambayo inafanyika kwa tuzo za kila siku) lakini anaweza kushinda zaidi ya mara moja tuzo za wiki kulingana na anavyozidi kucheza na kujikusanyia alama nyingi Zaidi. Ili kuondoa shaka, kila mshiriki atastahili kupata zawadi moja kwa kila droo inayofanyika na hivyo ana nafasi mbili za kushinda Tuzo (moja kwa kila droo).
10.8 Mdhamini ana haki ya kuzuia Tuzo hadi atakaporidhika kuwa mdai wa zawadi ni mshindi halisi, na ana haki ya kuomba uthibitisho ikibidi.
10.9 Mdhamini (pamoja na wawakilishi wake) ana haki ya kuchunguza tuhuma yoyote ya ulaghai, tabia mbaya au inayotia shaka, watumiaji na au hesabu, kwa hiari yake mwenyewe, wakati wa Promosheni, wakati wa kuchezesha Droo au baada ya washindi kuwa wametangazwa. Mdhamini ana haki, na ni hiari yake mwenyewe kuwathibitisha washiriki katika Promosheni bila kutoa taarifa kwa mshiriki.
10.10 Mdhamini ataomba washindi waridhie kwa kuandika jina, picha na mfanano unaotumika na kuchapishwa na Mdhamini kuhusiana na Promosheni hii kwa muda wa miezi 12 (kumi na mbili) baada ya kutangaza washindi. Washindi wanaweza kukataa kutumia majina yao, picha na mfanano wao na Mdhamini.
10.11 Kwa kushiriki katika hii promosheni washiriki wanaridhia kufuata vigezo na masharti yaliyo hapa.
10.12 Kwa kushiriki katika hii Promosheni washiriki wote wanatoa ridhaa yao kupokea vifaa mbalimbali vya masoko na matangazo kutoka kwa Mdhamini. Washiriki watapatiwa fursa ya “Kujitoa” kupokea mawasiliano haya.
10.13 Washindi wanakubali kuwa ni sharti la Promosheni kuwa ili kustahili kudai zawadi, mshindi atatakiwa kusaini ili kuthibitisha kuwa amepokea zawadi, na vilevile kama fidia au hati ya kusamehe madai kama ilivyoelezwa katika vigezo hivi.
10.14 Kwa kushiriki katika Chekecha Mkwanja mteja ameridhia Vodacom kutumia na kutoa data zake kwa wengine walioshiriki katika huduma ya Chekecha Mkwanja.
10.15 Mshiriki aliye na alama za juu anaweza kuwa mshindi wa kila wiki au mkubwa na washindi wa kila siku hupatikana kupitia mchakato wa bahati nasibu.
10.16 Ikiwa kwa sababu yoyote bidhaa au zawadi yoyote ambayo haijadaiwa au kukusanywa katika kipindi cha miezi mitatu (3) baada ya mshindi kuwasiliana, Vodacom ina haki ya kuchagua mshindi mbadala baada ya kupata muongozo kutoka mamlaka ya kudhubiti michezo ya bahati nasibu.