Maswali ya mara kwa mara

  1. Huduma ya Chekecha Mkwanja ni nini?
    Chekecha Mkwanja ni huduma ya kidigitali inayotolewa na Vodacom na inahusisha ujibuji wa maswali kutoka katika vipengele mbali mbali kama michezo,muziki,afya,sayansi na digitali. Wateja watakao jiunga na kujibu maswali kwa ufasaha watajikusanyia point na kuweza kujishindia zawadi tofauti tofauti.
     
  2. Mteja anapataje taarifa kuhusu huduma hii?
    Wateja hupata taarifa ya huduma ya Chekecha Mkwanja kupitia jumbe fupi za simu za mkononi, matangazo ya runinga, kurasa za mitandao ya kijamii za Vodacom Tanzania na Global Publishers.
     
  3. Jinsi gani ya kujiunga na huduma ya Chekecha Mkwanja?
    Kuna njia 3 vya Usajili:
    - SMS (Ujumbe Mfupi wa maandishi): Tuma neno Chekecha, Mkwanja kwenda 15914.
    - Kupitia menu ya Vodacom *150*00#
    - Kupitia linki itakayo kupeleka kwenye jukwaa la Chekecha Mkwanja
     
  4. Je kuna gharama gani za kujiunga na Huduma?
    Baada ya kujiandikisha, mteja atatozwa Tsh 300 na kupokea maswali 9. Huduma hii ina kipengele cha kuongeza swali la ziada na mteja atatozwa Tsh 99 kwa kila swali moja la ziada.
     
  5. Mteja anacheza vipi Chekecha Mkwanja?
    Mteja anacheza kwa kutuma kwa kutuma neno Mkwanja au Chekecha kwenda 15914 na atapokea swali la kwanza akijibu atapokea la pili na kuendelea adi maswali tisa yatimie.
     
  6. Mteja anajiondoaje kwenye Huduma?
    Mteja anajiondoa kwa kutuma neno STOPau ONDOA kwenda 15914
     
  7. Washindi wanapataje zawadi zao?
    Washindi wa siku watakuwa wanapata zawadi zao kila siku na washindi wa wiki watakuwa wanatangazwa kila ijumaa kupitia chaneli na magazeti ya Global Publishers.
     
  8. Zawadi gani zitatolewa kwenye droo?
    bonyeza hapa